HabariNewsTravel

Mgomo wa marubani wa shirika la ndege la Kenya airways waathiri sekta ya utalii.

Wadau wa utalii hapa nchini wanasema mgomo wa marubani wa shirika la ndege la Kenya airways unaoendelea kwa siku ya 3 sasa utaathiri pakubwa safari za watalii wa humu nchini na vile vile wa kimataifa wanaotarajia kutembelea sehemu mbali mbali nchini.

Aliyekuwa mwenyekiti wa shirikisho la kitalii nchini ambaye pia ni mwanachama wa bodi ya shirikisho hilo Mohamed Hersi amesema kuwa mgomo vile vile utaathiri sifa za shirika la kenya airways ambalo linatambulika kimataifa.

Akizungumza na meza yetu ya habari Hersi amehoji kuwa mgomo huo ambao umelemaza usafiri umegharimu pakubwa watalii hasa waliohitaji kurejea makwao.

Ametoa wito wahusika kuangazia suluhu ya haraka kumaliza mgomo huo.

BY EDITORIAL TEAM