HabariNews

Utamaduni umetumiwa kama mpango maalum wa kukomesha dhulma za kijinsia na kuleta uwiano na utangamano miongoni mwa jamii.

Mpango huo umezinduliwa na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za kibinadaam kwale kwa ushirikiano na mashirika ya kimataifa ya UN women na Search for common ground katika bustani ya mji wa Kinango ambapo kabila mbalimbali zimejumuishwa ili kuondoa tofauti za kikabila na mirengo ya kisiasa.

Kulingana na mashirika hayo hatua hio inalenga kuwapa kina mama na wasichana mazingira salama ya kuwasilisha changamoto za kimsingi zinazowakabili ili kupata nafasi bora za kujiendeleza katika jamii.

Yusuf Lule mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za kibinadaam la HURIA amelaani vikali vitendo vya dhulma vinavyotekelezwa kaunti ya kwale.

BY EDITORIAL TEAM