HabariNews

Shule ya upili ya wavulana ya Arabuko Sokoke eneo bunge la Ganze kaunti ya Kilifi imesemekana kufungwa.

Shule ya upili ya wavulana ya Arabuko Sokoke eneo bunge la Ganze kaunti ya Kilifi imesemekana kufungwa baada ya wanafunzi kuonyesha utovu wa nidhamu.

Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Laban Mwangemi wanafunzi hao waligoma kuhudhuria masomo ya asubuhi (PREPS) na kuvunja mataa ya shule hiyo.

Aidha Mwangemi ameelezea kuwa wanafunzi hao wametekeleza visa vingi vya utovu wa nidhamu kama vile kupatikana na lita 3 tatu za petroli na mengineyo.

Vile vile amesema kuwa hatua hiyo imelazimu bodi ya shule hiyo kuifunga shule hiyo huku wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajiwa kufanya mtihani wa kitaifa kutumwa nyumbani.

Wakati huo huo Mwangemi amesema kuwa hawajabainisha gharama kamili ya hasara waliosababisha wanafunzi hao ila tayari wamekwisha fukuza wanafunzi wanne baada ya kesi hiyo kuwasilishwa katika kituo cha polisi cha Ngerenya.

BY EDITORIAL TEAM