HabariNews

Familia moja Malindi yalilia haki baada ya mwili wa Mpendwa wao kubainika hauna viungo muhimu.

Ripoti ya upasuaji uliofanyiwa mwili wa Amani Justin Luwali aliyefariki katika njia tatanishi nchini Italia imebaini kuwa hauna baadhi ya viungo muhimu vya ndani ya mwili.

Upasuaji huo uliofanywa katika hospitali ya Rufaa ya malindi kaunti ya Kilifi, umeonyesha mwili wa Amani aliyefariki akiwa na umri wa miaka 35, hauna Moyo, mishipa mikubwa ya damu, figo, Mboni za macho, na ini.

Amani ambaye ni mkaazi wa Malindi anadaiwa kuolewa na mwanamme mmoja raia wa Italia na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike.

Kwa mujibu wa familia yake walifahamu kuhusu kifo cha mpendwa wao tarehe 27 mwezi septemba mwaka huu baada ya kupokea simu kutoka kwa jamaa anayeishi italia aliyewaarifu kwamba marehemu amefariki nyumbani kwake.

BY EDITORIAL TEAM