HabariNewsSiasa

Naibu Rais apata afueni baada ya mahakama ya kukabili ufisadi kufutilia mbali kesi dhidi yake.

Mahakama inayoshughulikia kesi za ufisadi nchini imekubali ombi la mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya Umma Noordin Hajj la kumuondolea kesi ya ufisadi wa shilingi bilioni 7.5 naibu rais Rigathi Gachagua na watu wengine 9.

Inadaiwa gachagua alijipatia pesa hizo kupitia akaunti yake ya benki ya Rafiki.

Stakabadhi zilisema kwamba kati ya mwaka 2013-2020, Gachagua alipokea pesa hizo kwenye akaunti zake 3 za benki hiyo, mashtaka ambayo DPP anasema hayana msingi wa kuyaendeleza.

Kesi hiyo imefutiliwa mbali kuambatana na kifungu 87 cha katiba ya nchi kwa kigezo kwamba imekosa Ushahidi.

Hakimu Victor Wakumile hata hivyo ameonya mshtakiwa kuwa huenda akakamatwa tena siku zijazo kwa makosa sawa na hayo iwapo kutakuwa na Ushahidi mpya.

BY EDITORIAL TEAM