Gavana wa Kwale Fatuma Achani ameyakosoa mashirika yanayojihusisha na maswala ya uvuvi kaunti hiyo kwa madai ya kuendeleza shughuli zao kwa manufaa ya kibinafsi.
Akizungumza katika eneo la Shimoni, Achani amedai kuwa mashirika hayo yamekuwa yakiendeleza miradi ya maendeleo isiyowafaidi wavuvi wa eneo hilo.
Gavana huyo amelalamikia hatua ya mashirika hayo ya kutohusisha viongozi wa serikali ya kaunti katika miradi hiyo inayolenga kuimarisha sekta ya uvuvi.
Kwa upande wake waziri wa madini na uchumi wa bahari Salim Mvurya ameyaagiza mashirika hayo kushirikiana na serikali ya kaunti hiyo ili kuhakikisha wavuvi wanafaidika na miradi hiyo.
Mvurya amewataka wasimamizi wa mashirika hayo kufanya kikao na gavana Achani ili kuelezea taratibu za utendakazi wa shughuli zao.
BY NEWS DESK.