Habari

Wazazi waombwa kuwapa watoto wao shughuli za kufanya msimu huu wa likizo.

Wito umetolewa kwa wazazi kuwapa watoto shughuli za kufanya msimu wa likizo kama njia ya kuwadhibiti kujihusisha na mambo yasiyofaa.

Kulingana na mtetezi wa haki za kijamii kwale Nuru Mohammed amedokeza kuwa kutokana na likizo ndefu ya Disemba watoto watakuwa na muda mwingi nyumbani jambo linalowapa nafasi hata yakuweza kujiingiza katika hulka mbovu .

Mohammed amewataka wazazi kutengeneza misingi ya watoto hao Kwa kujihusisha kufanya mambo endelevu katika jamii.

Aisha amewataka wazazi kuchukua nafasi hii kuwafundisha watoto kuhusu maswala ya fedha haswa ikilinganishwa kuwa kwa sasa gharama ya maisha iko juu.

Akisema kuwa ni taaluma ambazo zitawasaidia watoto hata siku za usoni wanapokuwa na kazi zao.

BY EDITORIAL DESK