HabariNews

Onyo Kali latolewa Kwa watakao jihusisha na udanganyifu wa mtihani.

Onyo Kali latolewa Kwa watakao jihusisha na udanganyifu wa mtihani kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Mwaka huu Watahiniwa 50,407 wa shule za msingi ndio watakao kalia mtihani wa kitaifa wa darasa la 6 na darasa la nane mtawalia katika kaunti ya Kwale.

Kulingana na mkurugenzi wa elimu kaunti ya Kwale Martin Cheruiyot watahiniwa elfu 25,913 watakalia mtihani wa darasa la sita KPSEA huku watahiniwa elfu 24,494 wakikalia mtihani wa KCPE.

Cheruiyot amesema kuwa kila mtahiniwa atapata nafasi ya kujiunga na shule ya upili na kuwataka wazazi kutokuwa na wasiwasi kwani serikali iko tayari kwa alama zozote atakazopata mwanafunzi.

BY EDITORIAL DESK