HabariNews

Maafisa wasimamizi katika kaunti ya Kwale watakiwa kuhakikisha watoto walemavu wanapata basari

Gavana wa Kwale Fatuma Achani amewaagiza maafisa wa kusimamia wadi kwenye kaunti hiyo kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata msaada wa basari ili kugharamia karo yao shuleni.

Achani amesema kuwa serikali yake imetenga fedha za basari kwa wanafunzi walemavu ikizingatiwa kwamba baadhi yao wanatoka familia maskini.

Gavana huyo ametoa agizo kwa maafisa hao kuwapa fedha hizo wanafunzi wenye ulemavu katika shule za msingi, upili na vyuo vikuu.

Haya yanajiri baada ya kubainika kuwa baadhi ya watoto walemavu wanasalia nyumbani kutokana na ukosefu wa karo.

Mmoja wa wazazi Lilian Kibe amedai kuwa watoto wenye ulemavu wamesahaulika katika maswala ya elimu licha ya baadhi ya wazazi kukosa karo.

BY EDITORIAL DESK