HabariNews

Zaidi ya familia 150 katika kijiji cha Nyango eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale zimepokea msaada wa chakula.

Zaidi ya familia 150 katika kijiji cha Nyango eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale zimepokea msaada wa chakula kutoka kwa muungano wa wahudumu wa utalii kaunti hiyo.

Mwenyekiti wa muungano huo John Baya amesema kuwa chakula hicho kilichogharimu takriban shilingi elfu 200 kitawasaidia kwa muda wakaazi wa eneo hilo wanaokumbwa na baa la njaa.

Baya amedokeza kuwa msaada huo unalenga kupiga jeki juhudi za serikali za kuwasaidia waathiriwa wa janga la ukame nchini.

Kwa upande wao wakaazi waliopokea unga wa sima, mchele na sukari miongoni mwa bidhaa nyingine wameupongeza muungano huo kwa kuwakumbuka.

Wakiongozwa na Mwangolo Dudu, wakaazi hao wamesema kwamba chakula hicho kitawasaidia wakati huu wa likizo ya Disemba.

BY EDITORIAL DESK