HabariNews

Ukosefu wa mahakama umetajwa kuchangia pakubwa visa vya dhulma za kijinsia katika eneo la Ndavaya.

Ukosefu wa mahakama umetajwa kuchangia pakubwa visa vya dhulma za kijinsia katika eneo la Ndavaya huko Kinango kaunti ya Kwale.

Kwa mujibu wa afisa wa maswala ya kisheria katika shirika la kutetea haki za kibinadamu (HURIA) Alex Mwarua, visa vya unajisi na mimba za utotoni vimekithiri kutokana na umbali wa mahakama.

Mwarua amesema kuwa visa hivyo vinalazimika kuishia kwa polisi kufuatia changamoto ya usafiri katika eneo hilo.

Kwa upande wake mkaazi wa eneo hilo Bakari Mainde amedokeza kuwa kesi hizo zinachukua muda mrefu mahakamani na kuathiri mchakato wa kutafuta haki kwa waathiriwa.

Haya yanajiri baada ya takriban kesi 11 za dhulma za kijinsia kuripotiwa eneo hilo katika siku za hivi majuzi.

BY EDITORIAL DESK