Wakaazi wa Nyango kutoka eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale wamelalamikia kero la uvamizi wa ndovu katika makazi yao.
Wakiongozwa na Regina Daudi, wakaazi hao wamesema kwamba wanahofia usalama wao baada ya watu watatu kujeruhiwa vibaya na ndovu.
Aidha, wenyeji hao wamesema kuwa ndovu hao wanavamia mashamba yao na kuharibu mimea wanayotegemea kupata chakula.
Kwa upande wake naibu msaidizi wa kamishna katika eneo la Ndavaya Charles Msila amesema kuwa ndovu wamekuwa wakitoroka katika hifadhi ya Kuranze inayopakana na sehemu hiyo kwa sababu ya ukame.
Msila amedokeza kwamba tayari wanashirikiana na shirika la uhifadhi wa wanyamapori nchini (KWS) ili kuwarudisha wanyama hao mbugani.
BY EDITORIAL TEAM