HabariNews

Wakaazi kutoka mjini Kwale walaumu idara ya usalama kaunti hiyo Kwa kuzembea katika utendakazi wao.

Wakaazi kutoka mjini Kwale walaumu idara ya usalama kaunti hiyo Kwa kuzembea katika utendakazi wao huku ikipelekea visa vingi vya utovu wa nidhamu kukithiri katika baadhi ya maeneo.

Wakiongozwa na Hamisi dawa amesema Kwamba zaidi ya visa 15 vya wizi huripotiwa huku ushirikiano baina ya askari na wakaazi ukiwa changamoto kubwa kwao.

Aidha ameeleza kwamba wamekua wakiripoti visa hivi lakini hawapati msaada wowote kutoka Kwa idara husika.

Kwa upande wake afisa katika shirika la utetezi wa haki za kibinadamu la human rights ajenda (Huria) mwinyihajj chamosi ameitaka jamii kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanaripoti visa hivi Ili haki iweze kupatikana.

BY EDITORIAL DESK