HabariNews

Bunge la kaunti ya Kwale limepitisha bajeti ya ziada ya shilingi milioni 25 zitakazotumika kuboresha huduma katika hospitali ya rufaa ya Msambweni.

Bunge la kaunti ya Kwale limepitisha bajeti ya ziada ya shilingi milioni 25 zitakazotumika kuboresha huduma katika hospitali ya rufaa ya Msambweni.

Mwakilishi wa wadi ya Ramisi Hanifah Mwajirani amesema kuwa fedha hizo zinalenga kuimarisha shughuli za utoaji matibabu katika hospitali hiyo.

Mwajirani ambaye pia ni kiongozi wa wengi katika bunge hilo amesema hatua hiyo itawawezesha wakaazi kupata huduma bora za afya.

Wakati uo huo, mwakilishi huyo ameeleza kuwa fedha hizo pia zitatumika kuwaajiri mabawabu ili kuimarisha usalama katika hospitali hiyo.

Mwajirani amedokeza kwamba mabawabu hao watashirikiana na askari wa kaunti ili kukabiliana na visa vya wizi vilivyokithiri katika hospitali hiyo.

BY EDITORIAL DESK