HabariNews

Shirika la msalaba mwekundu nchini limeafiki kupungua kwa asilimia 40 ya mikasa na majanga katika kaunti ya Kwale

Shirika la msalaba mwekundu nchini   limeafiki kupungua kwa asilimia 40 ya mikasa na majanga katika kaunti ya Kwale  mwaka uliopita ikilinganishwa na mwaka wa 2021 .

Mshirikishi wa shirika hilo Kwale Mohammed Mwaenzi ameitaja hatua hio kufanikishwa na ushirikiano kati ya shirika hilo, jamii na taasisi mbalimbali za serikali.

Mwaenzi akiafiki shirika hilo kujizatiti na kuwajibikia takriban visa vya ajali za barabarani 15 , visa 9 vya watu kufa maji , kesi 4 za moto ,uvamizi takriban kesi 10 , vifusi kesi mbili miongoni mwa mikasa mingineyo.

Hata hivyo amedokeza kwamba tayari maafisa wa msalaba mwekundu kwa ushirikiano na maafisa wa usalama na wale serikali ya kaunti ya kwale wameshika doria katika kila kona ya kaunti hio ili kuhakikisha wanakabiliana na visa vinavyolenga kuhujumu usalama wakati huu wa sherehe.

BY EDITORIAL DESK