HabariNews

Wazazi walaumiwa Kwa kuzembea katika jukumu la ulezi.

Wazazi walaumiwa Kwa kuzembea katika jukumu la ulezi na kuwacha watoto wao kujiingiza katika magenge ya kihalifu .

Haha ni kulingana na mufti mkuu Sheikh Omar Buya asema kuwa wazazi wengi hawajishughulishi katika malezi ya watoto wao kwa kuwa na shughuli nyingi za kimaisha na kusahau watoto wao.

Aidha ametoa wito kwa vijana kutojiunga na makundi ya kihalifu akisema kuwa uhuni haulipi bali unaweza kuwafanya hata kupoteza maisha yao.

Badala yake amewasihi vijana kutafuta shughuli zitakazo wajenga kimaendeleo na kuwapa mtaji wao wa kila siku kama vile biashara ndogo ndogo.

Ameyazungumza haya katika eneo la Ng’ombeni , Matuga kaunti ya Kwale.

Aidha katika siku za hivi majuzi eneo la Matuga limeshuhudia ongezeko la visa vya uhalifu kutoka kwa magenge ya vijana

BY EDITORIAL DESK