HabariNews

Serikali ya kitaifa na ile ya kaunti ya Kwale italazimika kuchukua hatua za haraka na kutoa msaada wa dharura kwa familia 82.

Serikali ya kitaifa na ile ya kaunti ya Kwale italazimika kuchukua hatua za haraka na kutoa msaada wa dharura kwa familia 82 katika eneo la Ndavaya huko Kinango kaunti ya Kwale baada ya kuathirika na kimbunga siku ya jumapili .

Kulingana na tathmini iliyofanywa na shirika la msalaba mwekundu kimbunga hicho kilibomoa paa za takriban nyumba 102 katika ya 170 zilizopo katika kijiji cha Ndavaya ,shule ya upili ya ndavaya na zahanati….

Waathiriwa sasa wakiendelea kuvumilia kibaridi kikali usiku kucha….Bakari Mainde ni mmoja wa waathiriwa hao

Akizungumza na wanahabari baada ya kukutana na waathiriwa hao wa kimbunga Kamishna wa Kwale Gideon Oyagi amesema kwamba kamati inashughulikia majanga kwale italazimika kufanya kikao maalum cha kuafikia mwafaka wa jinsi watakavyo wasaidia waathiri huku akiafiki serikali ya kitaifa tayari kutoa chakula cha msaada kwa waathiriwa.

Kwa upande wake naibu gavana wa Kwale Chirema Kombo amewaomba wahisani kujitokeza na kupiga jeki juhudi za serikali ya kaunti ya kwale za kuwasaidia waathiriwa.