HabariNews

Wakaazi  wa Ndavaya  eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale walalamikia tatizo la umeme.

Wakaazi  wa Ndavaya  eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale walalamikia tatizo la umeme sehemu hiyo Kwa muda mrefu hususan kunapotokea tatizo lolote katika kijiji hicho.

Kulingana na mmoja wa wakaazi Bakari Maiende  asema kuwa mara nyingi wao hulazimika kukaa gizani kwa hata zaidi ya miezi mitatu kunapokuwa na tatizo lolote huku kampuni ya umeme ya Kenya Power ikikosa kuwashughulilia haraka ipasavyo.

Akiongeza kuwa wanahofu baada ya mkasa wa kimbunga huenda wakalazimika kusubiri muda mrefu kabla ya umeme kuregea.

Hata hivyo kamishna wa kaunti ya Kwale Gideon Oyagi amewahakikishia wakaazi katika kijiji hicho kuwa umeme utaregeshwa mara moja tu baada ya shirika la Kenya Power kutathmini hali.

Akisisitiza kuwa watashirikiana na wakaazi kuona kuwa tatizo hilo linakabiliwa na wakaazi hawaendelei kupata hasara haswa katika biashara na sehemu ambazo zinahitaji umeme.

BY EDITORIAL DESK