HabariNews

Waathiriwa wa kimbunga huko ndavaya eneo bunge la Kinango watasaidika na chakula Cha msaada kutoka serikali ya kitaifa

Waathiriwa wa kimbunga huko ndavaya eneo bunge la Kinango watasaidika na chakula Cha msaada kutoka serikali ya kitaifa ambapo imetumana magunia 600 ya maharagwe na na 520 ya mchele.

Haya yanajiri huku washikadau na wahisani wakihimizwa kujitokeza kuwasaidia waathiriwa hao ili waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida.

Akizungumza katika kijiji cha Ndavaya baada ya kuzuru waathiriwa kamishna wa kaunti ya Kwale Gideon Oyagi amesema kuwa baada ya kutathmini hali wanatuma chakula kama hatua ya kwanza kuwasaidia waathiriwa.

Akiongeza kuwa eneo hilo pia limekuwa likishuhudia janga la njaa hivyo basi kushuhudiwa kwa mkasa huo umesababisha hatari zaidi ya baa la njaa.

Oyagi pia amesema kuwa serikali itatuma mahema kwa wakaazi ambao nyumba zao ziliharibika ili waweze kujistiri wakisubiri usaidizi zaidi wa maakazi  yaliyoharibiwa na kimbunga hicho.

Kwa upande wake naibu gavana wa kaunti hiyo Chirema Kombo amesema kuwa kando na chakula serikali ya kaunti itawapa basari wanafunzi wa kijiji hicho katika shule za upili kutokana na hali ngumu wanayopitia kwa sasa.

Kwa upande wake mbunge wa Kinango Gonzi Rai amesema kuwa watasaidia shule ya upili ya ndavaya ili kuhakikisha  wanafunzi wanaotarajiwa kufungua shule katika majuma mawili yajayo wataendelea na msomo bila usumbufu.

BY EDITORIAL DESK