HabariNews

ITS OVER!!! NASHA TRAVIS

Kuna uwezekano kuwa Nasha Travis msanii wa kike anayetokea pwani kutoshirikiana tena na Meneja wake wa awali almaarufu kama Nelson ambaye ni CEO wa Ba Nelson Empire.

Haya yanajiri baada ya meneja huyo wa miaka miwili kuchapisha katika mtandao wake wa whatsapp akisema “mwisho wa jambo moja ni mwanzo wa lingine, nilifurahi kufanya kazi na hii talanta kwa miaka miwili. Nakutakia kila la kheri.”

Nelson aliongeza kuwa atashirikiana na wasanii wawili wa kiume mwaka huu na kudokeza vigezo atakavyohitaji ili kufanya kazi nao.

Nelson vilevile amekuwa meneja wa msanii wa kike almaarufu kama Adasa japo kwa muda mfupi tu.

Ikumbukwe kwamba, Mnamo tarehe 19 Novemba mwaka 2022 Nasha Travis alidondosha kibao alichoshirikiana na msanii wa mziki aina ya Hiphop maarufu kama Katapilla kinachojulikana kama “ITS OVER”, je unadhani kuwa inaweza kuwa njia ya kukitrendisha kibao hicho?

Kibao chenyewe hiki hapa!

BY EDWIN KIPROTICH