HabariNews

Zaidi ya wazee 100 katika eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale wamekosa kupokea fedha zao zinazotolewa kila mwezi.

Zaidi ya wazee 100 katika eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale wamekosa kupokea fedha zao zinazotolewa kila mwezi na serikali kupitia mpango wa Inua Jamii baada ya mashine za kutambua vidole vyao kufeli.

Wakiongozwa na Thomas Nguli, wazee hao wamelalamikia kutopata fedha zao kwa wakati baada ya mashine hizo za kielektroniki kutofanya kazi kutokana na tatizo la kimtandao.

Imewalazimu wazee hao kutoka sehemu mbali mbali kusubiri kwa muda mrefu kupatiwa fedha hizo ambazo ni shilingi elfu 8 za tangu mwezi Julai.

Hata hivyo, wazee hao wameafiki kufaidika pakubwa na fedha hizo kwa kuwalipia karo wanao pamoja na kuwasaidia katika mahitaji mengine ya kinyumbani.

BY EDITORIAL DESK