Vijana wanaozuru fuo za bahari wamhimizwa kuwacha fuo hizo zikiwa safi kama wanavyozipata ikiwa ni njia mojawapo ya kulinda mazingira wanapokuwa ufuoni katika kaunti ya Kwale.
Kulingana na kiongozi wa vijana katika kaunti ya Kwale Hafswa Mohammed mara nyingi vijana wanaokwenda kujivinjari ufukweni hawatili maanani maswala ya kulinda mazingira hayo.
Ameongeza kuwa mara nyingi watu hufikiria ni jukumu la serikali kusafisha bahari ilihali wao ndio wamechafua mazingira hayo kwa plasitiki na uchafu mwengine.
Akisema kuwa mara nyingi sehemu ambayo ni nadhifu huvutia hatawatalii.
Mohammed amesema kuwa fuo za Kwale ni miongoni mwa fuo ambazo ni safi Pwani ya Kenya na hata zimepata tuzo kwa kuwa na mazingira bora.
BY EDITORIAL DESK