HabariNews

Visa vya wazee kuuawa kwa tuhuma za ushirikina vyashamiri Pwani.

Visa vya wazee kuuawa kwa tuhuma za ushirikina vimeendelea kushamiri licha juhudi za serikali kuu na mashirika ya kijamii kuvikomesha.

Familia ya Mohammed Nyamawi mzee mwenye umri wa miaka 62 sasa inadai haki baada ya mzee huyu kuuawa kwa kukatwa na panga tarehe 14 mwezi huu katika eneo la mwananyamala wadi ya Dzombo eneo bunge la Lunga Lunga kaunti ya Kwale.

Kulingana na Nyae Hassan Mwajoto ni kwamba walipata waraka ambao marehemu alikuwa ameandika vilevile ameongeza kuwa marehemu alipiga ripoti katika kituo cha polisi mwaka 2016 kwa kuhofia kuwa maisha yake yamo hatarini.

Idara za usalama aidha zimeelekezewa kidole cha lawama kwani kulingana na Julius Wanyama kutoka shirika la haki yetu ni kuwa utepepetevu wa idara husika zinachangia kwa ongezeko la visa vya mauaji ya wazee.

Shirika hilo sasa limezitaka idara husika kuingilia kati kuona kuwa wakaazi wa hamasa za utangamano zinatoelewa kwa waakazi pamoja na kubuni mbinu za kukabiliana na mauaji haya ya kiholela kwa wazee.

Visa vya wazee kuuawa kwa tuhuma za ushirikiano vimeendelea kushamiri licha juhudi za serikali kuu na mashirika ya kijamii kuvikomesha.

Familia ya Mohammed Nyamawi mzee mwenye umri wa miaka 62 sasa inadai haki baada ya mzee huyu kuuawa kwa kukatwa na panga tarehe 14 mwezi huu katika eneo la mwananyamala wadi ya Dzombo eneo bunge la Lunga Lunga kaunti ya Kwale.

Kulingana na Nyae Hassan Mwajoto ni kwamba walipata waraka ambao marehemu alikuwa ameandika vilevile ameongeza kuwa marehemu alipiga ripoti katika kituo cha polisi mwaka 2016 kwa kuhofia kuwa maisha yake yamo hatarini.

Idara za usalama aidha zimeelekezewa kidole cha lawama kwani kulingana na Julius Wanyama kutoka shirika la haki yetu ni kuwa utepepetevu wa idara husika zinachangia kwa ongezeko la visa vya mauaji ya wazee.

Shirika hilo sasa limezitaka idara husika kuingilia kati kuona kuwa wakaazi wa hamasa za utangamano zinatolewa kwa waakazi pamoja na kubuni mbinu za kukabiliana na mauaji haya ya kiholela kwa wazee.

BY JOYCE KELLY