Visa vya watu kuvamiwa na kukatwa kwa mapanga katika wadi ya Dzombo eneo bunge la Lungalunga kaunti ya Kwale vimetajwa kukithiri na kuwa jambo la kawaida.
Fredrick Mchombo ambaye kaka zake watatu wanauguza majeraha ya mapanga, anasema idara ya usalama imechangia pakubwa kwa ongezeko la visa hivyo kwani wanapopiga ripoti polisi wao hushauriwa kufanya kikao nje ya kituo na kutatua wenyewe visa hivyo.
Kwa upande wake afisa wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Yetu Julius Wanyama amesema utepetevu wa idara ya usalama unachangia ongezeko la visa hivyo kutokana na wahalifu kutochukuliwa hatua za kisheria.
Aidha wakaazi hao sasa wameitaka idara ya usalama kuwachukulia hatua za kisheria wale watakaopatikana na hatia ya kuwavamia wengine kwa silaha.
BY JOYCE KELLY