Wauguzi wakiadhimisha wiki ya manesi na kusheherekea huduma muhimu ambazo wamekua wakitoa kwa muda mrefu kwa wananchi, serikali za kaunti na ile ya kitaifa zimetakiwa kulishughulikia kwa haraka tatizo la uhaba wa wauguzi katika hospitali na vituo vya afya ya umma ili kuboresha huduma za afya.
Naibu mwenyekiti wa muungano wa manesi nchini Pauline Ngala amezitaka serikali za kaunti na ile ya kitaifa kuboresha miundo msingi na kuongeza wauguzi katika hospitali kuu akieleza kuwa hatua hiyo itaboresha utendakazi wa wauguzi.
Kwa upande wake mshirikishi wa afya ya uzazi kaunti ya Kilifi Kenneth Miriti ameitaka serikali kulichukulia swala la uhaba wa wauguzi kama janga na kuajiri wauguzi zaidi kudhibiti huduma zinazotolewa katika vituo na hospitali za serikali
Hata hivyo naibu gavana wa Kilifi Florence Mbetsa Chibule amewahakikishia wauguzi wa kaunti ya Kilifi kuwa lalama zao zitahughulikiwa huku akisistiza kuwa muda zaidi utahitajika kabla ya wauguzi walioshiriki mgomo wakati wa serikali iliyopita kulipwa marupurupu yao.
BY ERICKSON KADZEHA