Baadhi ya wabunge wanaoegemea mrengo wa Azimo katika bunge la kitaifa wameondoka Bungeni punde tu Waziri wa Hazina ya Kitaifa Prof. Njuguna Ndung’u alipoanza hotuba yake kabla ya kusoma makadirio ya bajeti yam waka 2023/2024.
Wakizungumza na wanahabari nje ya majengo ya bunge wabunge hao wakiongozwa na Kiongozi wa wachache Opiyo Wandayi na Kiranja wa wachache bungeni Junet Mohammed wamesema hawaiungi mkono bajeti hiyo inayosomwa sawia na mapendekezo ya mswada tata wa fedha ulivyopitishwa kwa kura 176 dhidi ya 81 za waliopinga.
“Tunaipinga bajeti hiyo haituhusu kwani imefeli kuangazia matakwa ya wananchi, kutokana na kupitishwa kwa lazima ripoti ya mswada tata wa fedha,” akasema Junet Mohammed, mbunge wa Suna Mashariki.