AfyaHabariNewsSiasa

SEKTA ZA ELIMU, USALAMA NA KILIMO ZANUFAIKA PAKUBWA NA MGAO WA BAJETI YA MWAKA HUU

Sekta za usalama, elimu na kilimo ni miongoni mwa sekta ambazo zimenufaika pakubwa kwa kutengewa bajeti ya juu mwaka huu wa kifdha wa 2023/2024.

Akisoma makadirio ya bajeti hiyo Waziri wa hazina ya fedha na mipango ya uchumi, Prof. Njuguna Ndung’u amesema sekta ya elimu imetengewa bilioni 630 ikiwa ni aslimia 27.4 ya bajeti nzima.

Fedha hizo zitafanikisha mipango mbalimbali ikiwemo mtaala wa umilisi CBC, kuajiri walimu zaidi na kufadhili elimu ya bila malipo kwa wanafunzi wa shule za msingi na upili.

Shule za sekondari msingi (Junior Secondary) imetengewa shilingi bilioni 25.5

Waziri Ndung’u amebaini kuwa serikali imeanza safari ya mageuzi ya kupunguza gharama ya maisha ya wakenya hasa wajasiriamali wa biashara ndogo na za wastani, kwa kuongeza fedha zaidi akisema bajeti hii inamfaa zaidi mwananchi wa kawaida.

Amesema ongezeko la fedha za ziada za bilioni 10 zilizowekezwa na serikali katika hazina ya Hasla zitapiga jeki juhudi za serikali kuwezesha ujasiriamali nchini.