MichezoSports

Samba Sports Youth Agenda yatumia michezo kuhamasisha jamii

Shirika la Samba Sports Youth Agenda linatumia mbinu ya michezo ya kuigiza, densi na mpira kama njia ya kuhamasisha jamii na haswa vijana kuhusu afya ya akili na kujitoa uhai

Akizungumza wakati wa hamasa kuhusu afya ya akili katika eneo la Kombani kaunti ya Kwale afisa wa mipango wa shirika la Samba SPORTS Youth Agenda Mwanaisha Kuwania anasema kuwa michezo ya kuigiza inafana katika hamasa hiyo kwani watu wengi hupenda kutumbizwa huku wakielimishwa.

Nasra Mohammed Mwajora ni muigizaji na anasema kuwa wanatumia sanaa ili kufunza jamii kuhusu athari ya kujitoa uhai na msongo wa mawazo.

Kwa upande wake Dan Kinyanjui ambaye ni msanii na pia muathiriwa aliyepitia tatizo la msongo wa mawazo ameitaka jamii kutowabagua wanaopitia hali hiyo.

Akitoa wito kwa waathiriwa kujikubali ndio mwanzo wa kupata nafuu katika afya ya kiakili.

Aidha muuguzi mtaalam wa maswala ya akili na mshauri nasaha Triza Ireri akitaka wanaohisi kuwa na matayizo ya kiakili kutafuta ushauri mara moja.

BY EDITORIAL DESK