MichezoSports

MASHINDANO YA DUNIA YA TAE KWON DO NCHINI MEXICO

Patrick Lolkalepi kutoka Kilifi Tae Kwon Do Club iliyo katika kijiji cha Kibaoni mjini Kilifi na mwenzake Peter Kabane kutoka eneo la Mtwapa, kaunti ya Kilifi kwa mara ya kwanza wamepata fursa ya kuiwakilisha Kenya kwenye mashindano ya PARA WORLD TAE KWON DO CHAMPIONSHIP makala ya 10 yatakayoandaliwa nchini Mexico.
 
Wawili hao wamejumuishwa kwenye timu ya taifa baada ya kufuzu kwenye michuano ya mchujo iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha mafunzo ya askari wa magereza mjini Ruiru kaunti ya Kiambu.
 
Kulingana na kocha wa Lolkalepi, Micheal Akida Sifa ni kuwa licha ya mchezaji wake kushiriki michuano ya mchujo kwa mara kwa kwanza, weledi aliouonesha ni wa kiwango cha juu.
 

Kwa upande wake Lolkalepi, ameeleza matumaini yake ya kufanya vyema na kuleta taji nyumbani, huku akitoa changamoto kwa vijana wengine walio na uatilifu kujikubali na kujitokeza ili kuendeleza talanta zao.

Kikosi cha timu ya taifa kinatarajiwa kuingia kambini jijini Nairobi kwa mazoezi zaidi kabla ya kusafiri nchini Mexico kwa mashindano.

BY ERICKSON KADZEHA