HabariNews

VIONGOZI WATAJWA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA SWALA LA UNYAKUZI WA ARDHI

Kwa miaka mingi tatizo la unyakuzi wa ardhi hasa eneo la ukanda wa Pwani halijapata utatuzi, wananchi wengi wakifurushwa kutoka kwenye makaazi yao ya muda mrefu.
 
Ila sasa lawama hiyo ya unyakuzi wa ardhi imeelekezwa kwa viongozi kwa kufeli kutafuta mbinu za kukabiliana na changamoto hiyo ili kukomesha mahangaiko kwa wananchi.
 
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa chama cha mijikenda cha Taireni, Peter Ponda ni kuwa matatizo ya ardhi hayawezi kutatuliwa na viongozi wa siasa kufuatia kuhusika kwao katika unyakuzi huo.

Aidha amesistiza kuwa chama hicho kwa ushirikiano na wananchi wamekuwa wakielekea mahakamani kupinga unyakuzi wa ardhi ukanda pwani ikiwemo ardhi ya shamba la Chakama, Giriama Ranch na ardhi nyingine kaunti ya Kwale.
 
Ameeleza kustaajabishwa kwake na hatua ya serikali kuwapa nyadhifa za uongozi baadhi ya viongozi ambao wanakabiliwa na kashfa za unyakuzi wa ardhi.

BY ERICKSON KADZEHA