AfyaHabariNews

Tatizo la Afya ya Akili ni Kero la Kitaifa na Kimataifa

Wataalamu wa afya ya akili wametaja ukosefu wa mafunzo ya afya ya akili kwa wahudumu wa afya kuwa miongoni mwa sababu zinazolemaza vita dhidi ya tatizo la afya ya akili nchini.

Margaret Kadzo Rubene mtaalamu wa afya ya akili amedokeza kuwa, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilifanya utafiti kuhusu tatizo hilo ambalo linaendelea kuwa sugu katika jamii.

Amesema utafiti huo ulibainisha sababu mbalimbali zinachangia watu wengi kukosa huduma mwafaka za afya ya akili mbapo wahudumu wa afya hasa ambao bado wako kwenye majaribio ya kimatibabu hawana ufahamu kuhusu afya ya akili.

“Kuna gap kubwa sana ambayo ilipatikana, kuwa wale watu ambao wako na shida za kiakili ndio wanapata hizi services za mental health. Kukatokea mambo kadha wa kadha ambayo yanasababisha hii gap. Kwa hivyo moja wapo ilikuwa ni hiyo ya kuwa madaktari hawana ule ujuzi,” Margaret amesema.

Kutokana na hali hiyo kuonekana kuwaathiri idadi kubwa ya wakenya, wadau mbalimbali wamejitokeza kuizungumzia.

Mkewe Naibu wa Rais Bi Dorcas Gachagua alilitaja afya ya akili kuwa janga kama janga la corona duniani. Kulingana Bi. Dorcas kuna haja kwa jamii na wataalamu kuzungumzia afya ya akili na kupunguza unyanyapaa pamoja na ongezeko la waathiriwa katika jamii zetu.

“Inatuathitiri sote na kile tunachojaribu kufanya ni kuleta uhamasisho kuhusu tatizo hili ambalo tuko nalo. Kwanza, ni janga hasa kama vile la Covid-19 ambapo inavuka mipaka, liko kila mahali, ni janga la ulimwengu na kile tunajaribu kusema ni kuleta uhamasisho ili suala hili watu wasilifanyie unyanyapa…,” alisistiza Bi. Dorcas.

Ili kukabiliana na janga hilo kikamilifu, Mtaalamu Kadzo amesema kuna haja kwa serikali kubuni mikakati ya kukabiliana na hali ngumu ya maisha pamoja na majanga ibuka.

Ameeleza kuwa kuwa gharama ya juu ya maisha na hali ya watu kushindwa kukidhi baadhi ya mahitaji yao pamoja na wale wanaowategemea ni moja ya sababu.

BY EDITORIAL DESK