Jaji aliyezuia kutekelezwa kwa Sheria tata ya Fedha ya mwaka 2023 ni miongoni mwa majaji 13 ambao wamehamishwa.
Jaji Mugure Thande ambaye alitoa uamuzi wa kusitisha utekelezwaji wa Sheria ya Fedha BAADA YA KESIkuwa akiongoza kitengo cha Kikatiba katika Mahakama ya Milimani jijini Nairobi amehamishiwa hadi Mahakama ya Malindi kaunti ya Kilifi.
Wengine walioathiriwa na mageuzi hayo ni hakimu Chacha Mwita akiteuliwa kuongoza Kitengo cha Kikatiba kama jaji msimamizi.
Uhamisho mwingine mkubwa ni wa Jaji Diana Kavedza ambaye hivi karibuni amepandishwa cheo na kuwa jaji wa mahakama kuu kutoka kwa hakimu aliyekuwa akiongoza mahakama ya Kahawa.
Kando na majaji ho mwengine aliyehamishiwa hadi kitengo na idara nyingine ni Jaji David Majanja anayesikiliza kesi kuhusu uhalali wa Sheria ya Fedha mwaka 2023 ambaye amehamishwa kushughulia kitengo cha Umma.
Hii hapa orodha ya majaji wengine waliohamishwa