HabariLifestyleNews

Raia wa Ujerumani Ahukumiwa Miaka 81 Gerezani

Raia mmoja wa Ujerumani amehukumiwa kifungo cha miaka 81 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya ulanguzi wa binadamu.

, kujihushisha na ngono za watoto pamoja na kuendeleza vitendo visivyo sahihi kwa watoto.

Thomas Scheller mwenye umri wa miaka 73 mnamo Jumanne, Agosti 8 alikutwa na hatia ya kutekeleza hayo pamoja kujihusisha na ngono za watoto na kuendeleza vitendo visivyo sahihi kwa watoto.

Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Milimani Caroline Njangi akisoma uamuzi huo alisema shtaka la kushiriki ngono za watoto linapelekea kigfungo cha zaidi ya miaka 7.

“Kosa la kujihusisha na ngono ya watoto lina kifungo cha miaka 7 na miaka 7 kwa kila kosa la nne, tano, sita, hata hivyo Mshukiwa ana haki ya kukata rufaa ndani ya siku 14 na atawekwa katika rejista ya wahalifu wa ngono waliohukumiwa,” alisema Hakimu.

Inaaminika kuwa Scheller aliingia nchini kinyume cha sheria na alimnajisi msichana mwenye umri mdogo huko Nyalenda kaunti ya Kisumu kati ya mwezi Machi na Aprili mwaka wa 2020 miongoni mwa matukio mengine.

Schiller pia anasemekana kutorokea Kisumu alipokamatwa na maafisa wa usalama baada ya kutekeleza vitendo sawia hapa Pwani.

Licha ya Scheller kujitetea kwa kusema kuwa alisingiziwa mambo hayo na kuitaka mahakama kumuonea huruma, mahakama hiyo imeshikilia uamuzi huo kwa kuzingatia ushahidi uliowashilishwa mbele ya mahakama hiyo.