HabariNews

Vijana wahimizwa kujitokeza kunufaika na fedha walizotengewa.

Viongozi kwa ushirikiano na serikali za kaunti na ile ya kitaifa wametakiwa kuwahamasisha vijana nchini ili wanufaike vilivyo na fedha wanazotengewa kuwanufaisha.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la vijana la Stretchers kaunti ya Mombasa Dickson Okong’o ameeleza kuwa licha ya serikali kuzindua mipango maalum ya fedha inayolenga vijana na makundi mengine nchini, bado kuna vijana ambao hawafahamu jinsi ya kunufaika na fedha hizo.

Kulingana na Okong’o ukosefu wa mafunzo pamoja na kile alichokitaja kama kuchelewa kwa fedha hizo kuwafikia baada ya kutuma maombi ni miongoni  mwa sababu zinazochangia vijana kutofuatilia fedha hizo.

“Asilimia kidogo ya vijana wanajitokeza na kunufaika na zile fedha, maybe sababu yawezakuwa labda wale vijana hawajapata mafunzo ya kutosha kuelewa ni vipi wanweza kuapply ile fedha wakaipata,” alisema Okong’o.

Okong’o ametoa wito kwa vijana kufuatilia na kuwatambua maafisa mbalimbali wanaoshughulikia masuala ya vijana ili kupata mafunzo na njia za kunufaika.

“ Vijana ni lazima tuhakikishe kwamba huu ni wakati lazima zile fedha amazo ziko za vijana tujitokeze, kuna maofisaa wa vijana kwa kila Sub- County , kama kijana itakuwa ni jambo la kusikitisha kwamba hujui ofisaa wako wa vijana ni nani.

So tafadhali chukuwa jukumu lako umjue ofisaa wako wa vijana ili muulize maswali mengi ni vipi mnawezakuendelea kibiashara,”alihimiza okong’o.

Mwenyekiti  wa bodi ya biashara na maendeleo ya vijana nchini Fatma Bakari Barayan amekariri mara kwa mara umuhimu wa vijana kutumia fursa hiyo pamoja na kujiunga katika makundi ili wanufaike na kujiendeleza kimaisha kupitia kwa fedha hizo.

BY MAHMOOD MWANDUKA