HabariNews

Familia moja Malindi kaunti ya Kilifi yaomba msaada wa kupata mwanao aliyejirusha baharini.

Familia Moja mjini Malindi kaunti ya Kilifi inaomba wahisani kujitokeza kuwasaidia kuokoa mwili wa mpendwa wao anayesemekana kuzama katika Kivuko cha Kilifi

Beatrice Neema Kalume Mwenye umri wa miaka 22 ambaye alikuwa mwanafunzi katika taasisi ya mafunzo ya walimu wa Shanzu alidaiwa kutoweka nyumba siku ya alhamisi alfajiri wiki Jana bila kuarifu jamaa zake alikokuwa akielekea.

Kulingana na mamae Mary Mwandodo baada ya kumtafuta kwa mda alielezwa na chifu wa eneo hilo kwamba kunamsichana ambaye alijitoa uhai kwa kujirusha kwenye maji.

Hata hivyo mama huyo alithibitisha kwamba ni mwanawe.

Tunamuangalia hivi huku hayuko huku hayuko, ndio yule Karani akachukua piki piki kumfuata akamkosa ndio basi ashaenda,tukapigiwa simu na chifu wa Malindi akasema kumejirusha mtu kwa maji kule bridge Kilifi kwa sababu alikuwa amewacha simu yake hii hap ana kitambulisho chake Bertice  Neema Kalume, ndio tukaja Kilifi kumuangalia, simu yake iko hap ana kitambulisho kiko hapa lakini bado sijampata”, alisema mama mwendazake.

Familia hiyo ilisema wavuvi wamekuwa wakiwasaidia kuutafuta mwili huo bila mafanikio.

BY EDITORIAL DESK