BurudaniEntertainment

Mpishi Stadi, Maliha aweka Rekodi Mpya ya Upishi wa muda Mrefu

Mpishi Hodari na maarufu aliyeingia katika rekodi ya vitabu vya kumbukumbu vya Guiness Maliha Mohammed amevunja rekodi nyingine tena kwa kupika kwa muda mrefu zaidi.

Maliha Mohammed amevunja rekodi kwa kupika kwa saa 95, dakika 15 akiwa amevuka rasmi rekodi ya awali iliyokuwa ikishikiliwa na mpishi wa marekani Rickey Lumpkin ambaye alipika kwa muda wa saa 68, dakika 30 na sekunde 1 Desemba 2018.

Maliha alianza mapishi hayo tarehe 10 Agosti na kuweka rekodi hiyo mpya.

“Ndio, tumefanikiwa! Mshindi mpya wa Rekodi ya dunia ya kupika kwa muda mrefu mjini! Shukran kwa kuniunga mkono!” Aliiandika kwenye mtandao

Ametoa shukrani zake kwa wafuasi wake ikiwemo Nadia Mukami, Crazy Kennar, Oga Obinna, Winnie Odinga kwa kumuunga mkono kwenye upishi huo.

Mafanikio makubwa ya mpishi huyo sasa yanangojewa kuthibitishwa na Guinness World Records, mchakato unaohusisha uthibitishaji wa kina na uhifadhi wa nyaraka.

Haya yanajiri baada ya mpishi wa Nigeria Hilda Baci kuthibitishwa mnamo mwezi Juni na Guinness World Record kama mmiliki mpya wa rekodi hiyo.

BY EDITORIAL DESK