HabariNews

Zoezi la utafiti wa madini lakamilika Kwale.

Vijiji 2 kati ya 6 ambavyo vinafanyiwa utafiti wa kupata madini ya Titanium katika eneo la Msambweni kaunti ya Kwale havijapatikana na raslimali  hiyo.

Haya yanajiri baada ya zoezi hilo kukamilika huku kampuni ya kuchimba madini ya Base Titanium ikiendeleza hamasa katika vijiji hivyo.

Akizungumza katika kijiji cha Magaoni afisa wa maswala ya kijamii kutoka kampuni ya Base Titanium Ali Masemo alisema zoezi la utafiti litasimamishwa katika vijijini hivyo.

Masemo aliongeza kuwa sema kufikia sasa wakaazi katika vijiji vyote wamekubali utafiti huo kuendelea na katika vijiji ambavyo madini yamepatikana wanatarajia kufanya awamu ya pili ya utafiti huo.

Wakaazi katika vijini vya Magaoni wakiongozwa na Ali Kassim Mwamakazi na Ramadhan Abdallah walisema wameridhika na zoezi hilo.

BY EDITORIAL DESK