HabariNews

Watu 3 watoweka baada ya kuvamiwa na Alshabab Lamu

Watu watatu hawajulikani waliko baada ya gari walomokuwa wakisafiria kuvamiwa na washukiwa wa kundi la kigaidi la Alshabab kwenye Barabara kuu ya Lamu-Witu-Garsen mapema Leo.

Inasemekana magari yanayotumia Barabara ya Mombasa Kwenda Lamu viloe vile yamevamiwa na wanamgambo hao katika eneo la Koreni.

Duru za habari ziliarifu kuwa gari moja aina ya Toyota Probox limeshambulikwa kwa risasi wakati wa tukio hilo.

Katika kisa hicho dereva wa gari moja alijaribu kukwepa washambuliaji na kushindwa kulidhibiti hatimaye kuingia kwenye kichaka ambapo kufikia sasa watu 3 waliokuwa ndani ya gari hilo hawajulikani waliko.

Wanajeshi wa KDF wanaendelea na msako kuwatafuta wahusika wa shambulizi hilo la kigaidi amabo wanaodaiwa kutorokea msituni

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa kukishuhudiwa visa vya mashambulizi ya kigaidi katika kaunti ya Lamu ambapo vile vile watu kadhaa wamepoteza maisha

Mwisho

BY EDITORIAL DESK