FunMichezoSports

Wasimamaizi wa Mechi baina ya Man Utd na Wolves Wasimamishwa

Wasimamizi wa mechi ya ufunguzi baina ya Man United na Wolves wamebanduliwa katika orodha ya watakaosimamia mechi za raundi ya pili ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kuwanyima Wolves penalti ya wazi.

Refarii Simon Hooper na wasaidizi wake kutoka kitengo cha VAR Micheal Sailsbury na Richard West walifumbia macho kitendo cha kipa Andre Onana kucheza visivyo katika boksi katika za lala salama za ngarambi hiyo.

Uamuzi huo umezua hisia kali miongoni mwa mashabiki mitandaoni ambao wanahisi wasimamizi hao walifanya uamuzi huo kwa makusudi.

“Itasaidia nini sasa, wawape Wolves pointi 1,” mmoja aliandika.

Mwengine shabiki wa Manchester United naye aliandika, “Hii ni kutaka kutuhujumu sana, VAR Card imekuja mapema sana sasa ona vile tutakavyokaziwa na waamuzi kwenye mechi zijazo.”

Hata hivyo waamuzi hao wameamrishwa kuomba msamaha kufuatia uamuzi wao ambao kwa mtizamo a wengi ulibadilisha mwelekeo wa matokeo ya ngarambe hiyo.

Mambo yalikuwa kinyume na matarajio ya mashabiki wa Manchester United ambao matumaini yao ya kujizolea ushindi mwepesi walipochuana na Wolverhampton Wanderers nusura kugonga mwamba.

Red devils walilazimika kusubiri hadi dakika ya 78 kupata goli lao la ushindi lililotiwa kimyanoi na difenda Rapha Varane kujibu pasi safi iliypopikwa na beki wa kulia Aaron wan Bissaka.

Manchester United watarejea uwanjani siku ya Jumamosi katika mechi yao ya pili watakapochuana na Tottenham Hotspurs.

BY SPORTS DESK