HabariNews

“Najivunia kushiriki Katika historia ya upatikanaji wa ugatuzi” Ruto

Ni kweli kuwa ugatuzi umekumbwa na vikwazo kadha wa kadha vilivyopelekea uratibu na maendeleo duni, ugumu wa kiutawala na ukosefu wa ufanisi mzuri kwenye utendakazi.

Ni kauli yake Rais William Ruto akiongea kwenye ufunguzi wa kongamano la nane la ugatuzi lililoandaliwa mjini Eldoret Kaunti ya Uasin Gishu, mnamo Jumatano, Agosti 16.

Rais alitataja ucheleweshwaji wa mgao wa fedha kwa serikali za kaunti, imesababisha maendeleo mabaya na kulemaza shughuli muhimu za ugatuzi.

“Kuna mengi ya kufanya na changamoto tele zimekuwepo hadi leo hii ugatuzi unakosa kuwa na umuhimu kwa wakenya wengi, ni kweli kuwa ugatuzi umepitia vikwazo tele ambavyo vimepelekea ugumu wa kuendeleza kaunti,” Alisema Rais.

Wakati huo huo amesema uongozi wake utakuwa imara na mstari wa mbele kuendeleza uongozi bora kwa kuziba mianya ya ufisadi akizitaka kaunti zisiwe sababu za kuendelea sakata za ufisadi.

“Nimejitolea katika uongozi wangu uwe msingi imara wa maendeleo, hatutaruhusu ufisadi. Na nazihimiza kaunti zisiwe msingi wa kuendeleza Sakata za ufisadi,” alisisitiza Kiongozi wa nchi.

Rais vile vile ameeleza kujivunia kuchangia upatikanaji wa ugatuzi nchini baada ya katiba mpya kuzinduliwa mnamo Agosti 27 mwaka 2010.

“Nimetokea kuwa sehemu ya historia hii, nilibahatika kushirki kwenye mazungmzo haya, na nafurahi sana kuwa leo tunasherehekea miaka 10 ya ugatuzi,” alisema Rais.

BY EDITORIAL DESK