AfyaHabariNews

Si aibu! Vijana wa Kiume wafahamishwe kuhusu Hedhi

Kuna haja ya vijana wa jinsia ya kiume kupata mafunzo kuhusiana na maswala ya hedhi kama njia moja ya kuepukana na aibu.

Mkurugenzi kutoka shirika la Together  4 Society Edwin Shamir  alionyesha haja ya wanaume kuwa na ufahamu kuhusu maswala ya hedhi na kwamba hedhi ni kitu cha kawaida miongoni mwa wanawake wala sio chaguo.

Aidha Shamiri aliongeza kuwa serikali inafaa kuwa mstari wa mbele kuendeleza elimu ya hedhi miongoni kwa wanaume katika umri mdogo ili anapokua mkubwa awe na ufahamu kuyahusu.

“Nadhani ni wakati mwafaka hata kwa serikali kuangalia aibu wanayopata wasichana wadogo wakati wa siku zao za hedhi na linafaa liwe jukumu la kila mwanaume kufahamu mambo ya hedhi katika umri mdogo mtoto anapoanza kujielewa.” Amesema Shamir.

Shamir alieleza kuwa hatua hiyo itawawezesha mwanaume kujua hali wanazopitia wanawake na kuwasaidia pale papohitajika.

Wakati huo huo Shamir alisisitiza kuwa ukosefu wa sodo  miongoni mwa wanafunzi wa kike bado ni changamoto hali ambayo huathiri masomo yao hasa kwa wale ambao wazazi wao hawajakubali kuwa hedhi ni jambo la kawaida huku akiitaja mojawapo ya sababu zilizoathiri elimu ya mtoto wa kike.

Ukosefu wa sodo unachangiwa mara nyingi na wazazi kokosa hasa wale ambao hawajakubali hedhi ni jambo la kawaida wengine wanadhani hedhi ni jambo la kujitakia.” Alisisitiza Shamir.

Shamir  alielezea  kisa cha mzazi aliweza kumpiga na kumjeruhi mtoto wake baada ya kumwambia kwamba yuko kwa siku zake za hedhi na anahitaji sodo jambo ambalo alilikemea vikali.