HabariNews

Uhaba wa shule watatiza masomo Voi

Huku Serikali ikizidi kuongeza Zaidi juhudi zake kuimarisha viwango vya elimu bora kwa kila mtoto nchini, bado kunashuhudiwa Ongezeko la wanafunzi kusaka masomo mbali na maeneo yao.

Wadi ya Kaloleni mjini Voi imeathirika pakubwa katika sekta ya elimu. Kulingana na mbunge wa Voi Abdi Chome wadi hiyo ina shule moja pekee ya sekondari yenye wanafunzi 21.

Uhaba huu umetatiza shughuli za masomo na kupelekea wanafunzi kuhamia maeneo mengenine kutafuta elimu ya sekondari licha ya kuwa eneo hilo linaongoza kwa idadi kubwa ya watu katika kauti ya Taita Taveta.

              “ Tuko tu na shule ya secondary ambayo ni moja na ina wanafunzi ishirini na moja, ili ifuatane na wengine tujaribu kwanza, sababu fedha ni ndogo lakini kwa uchache ndani ya muhula huu, wadi ya kaloleni  ipate shule za sekondari mbili mpya”  Alisema.

Aidha mwakilishi wadi Mbololo Azhar Din ameahidi kushirikiana na mbunge huyo ili kufanikisha ujenzi wa shule hizo na kuwapunguzia gharama kwa wazazi wanaolazimika kuwapeleka watoto wao shule za mbali kupata elimu.

 “ Namuunga mkono mia kwa mia na mimi nitampatia sapoti yangu pale anapotaka ili tuhakikishe ndani ya Kaloleni hii tuna shule mbili ama tatu za sekondari”  Alisema .

Ili kufanikisha malengo hayo, Chome hata hivyo alihidi kushirikisha na kupokea maoni ya wakaazi wa eneo hilo.

BY EDITORIAL DESK