HabariNews

Rais Ruto Amteua DPP Mpya Renson Mulele

Rais William Ruto amemtua rasmi Renson Ingonga Mulele kama Mkurugenzi mkuu wa wa Mashtaka ya Umma kuchukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Noordin Hajj.

Kupitia ripoti ya gazeti rasmi la serikali, Rais ruto amebaini kuwa Ingonga atahudumu katika ofisi hiyo kwa mda wa miaka nane.

Hatua hii inajiri wiki moja tu baada ya Wabunge kuidhinisha uteuzi wake katika zoezi kali la uhakiki. Katika ripoti ya zoezi hilo, kamati ilipendekeza kuteuliwa kwake kwa kuzingatia ufahamu wake katika masuala ya umma na utendajikazi wake alipohudumu kama msaidizi wa mkurugenzi wa mashtaka ya umma hapo awali.

Noordin Haji kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS).

BY EDITORIAL DESK