HabariNews

Mamlaka ya Bandari KPA Yakanusha madai ya kubinafsishwa kwa bandari ya Mombasa

Mamlaka ya Bandari nchini KPA imepuuzilia mbali tetesi kuwa kuna njama sehemu ama baadhi ya shughuli za bandari hiyo imebinafsishwa na serikali.

Mwenyekiti wa Mamlaka hiyo Benjamin Tayari amekana madai hayo na kutaja kama uzushi, akibaini kuwa lengo la KPA ni kukodisha baadhi ya sehemu za Mamlaka hiyo kwa wafanyabiashara na wala si kubinafsisha sehemu hizo kama inavyodaiwa.

Akizungumza katika kikao na wanahabari makao makuu ya Tayari ametetea hatua hiyo ya kukodisha sehemu hiyo na kusema kwamba kamwe haitaathiri utendakazi wa bandari.

“Zile habari za kusema bandari ya Mombasa inauzwa kuana tofauti kubwa ya kubinafsishwa na kukodishwa, tunakodisha mtu afanye biashara na sisi tunapata na hakuna kazi ambayo itapotea katika wale wafanyikazi ambao wanafanya kazi hapo.”Alisema Bw.Tayari

Tayari aidha amedokeza kuwa hatua hiyo itachangia katika uzalishaji wa nafasi zaidi za ajira bandarini pamoja na kuzalisha mapato zaidi kwa taifa la Kenya kupitia shughli za bandari.

“Tutakuwa na wafanyikazi wengi zaidi itakuwa ni faida kubwa kwetu na katika ulimwengu mzima kwa hivi sasa bandari zote zinaenda kwa ule mpango wa mamalaka wa bandari inasimamia bandari halafu wafanyibiashara wanakuja kufanya biashara a sisi tunapata mapato hapo.” Aliongeza Tayari.

BY EDITORIAL DESK