HabariNews

IEBC yapendekeza kukaguliwa kwa matokeo ya Uchaguzi ya Mwaka jana, 2022

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC imewasilisha mapendekezo yake katika katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo ukumbi wa Bomas jijini Nairobi.

IEBC ikiwa miongoni mwa makundi yaliyowasilisha mapendekezo yake, mnamo siku ya Ijumaa Septemba ikitaka masuala kadha wa kadha kushughulikiwa yakiwemo suala la Tume hiyo kufanyiwa mabadiliko miongoni mwa masuala mengine.

Mbele ya kamati hiyo Tume hiyo imependekeza kukaguliwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais mwaka uliopita, suala la uwakilishi wa kijinsia kutekelezwa ipasavyo, na vile vile swala la uratibu wa mipaka.

Vile kuangaziwa kwa suala la usalama wa makamishena wakati wa uchaguzi ambapo IEBC imelalamika kudhulumiwa na hata kuuawa kwa makamshina wake wakati wa uchaguzi mkuu.

Katika kikao hicho Upade wa Azimio umeataka kujua ni nani anayesimamia uchaguzi nchini, ambapo Tume hiyo kupitia Afisa Mkuu mtendaji wa IEBC Marijan Hussein Marijan akisema uchaguzi husimamiwa na makamshina na Mwenyekiti wa Tume huku nafasi yake ikiwa ni kuhakikisha shughuli zinaendelea vyema.

“Matokeo haya ya uchaguzi yalikuwa yakisimamiwa na makamishna na Mwenyekiti na kama ulitambua kuwa hakuna hata wakati mmoja makatibu wa tume walitangaza matokeo. Na langu ni kuhakikisha mchakato huo unafanya kazi vizuri na sambamba, kuwa na hatimaye wachukue jukumu la kuthibitishwa na kutangazwa ya matokeo,” alisema Marijan.

Na kuhusu mgawanyiko wa makamishna ulioshuhudiwa wakati wa kutangaza matokeo ya urais ya mwaka 2022, Marijan amesema mgawanyiko huo ni kutokana na mvutanao ulitokana na ukaribu wa kura za wagombea wakuu hivyo makamshina walipinga kushinikiza kutangazwa kwa duru ya pili ya uchaguzi.

“Utasemaje kuhusu mgawanyiko wa makamishna 4 ulitokea, kipi tukiamini?” Aliulizwa.

“Mara tu kundi moja walipoyaona matokeo walisema mwanya ni mdogo sana hatuwezi kuruhusu hilo, sikutarajia kuwa iwapo kamishna ana shauku hakuridhishwa na anataka uhakika wa matokeo hao tutasema kwa mfano tungealia kaunti hii kituo fulani cha kupigia kura kwa sababu walikuwa nyanjani,” alisema Marijan.

Kamati hiyo ya mazungumzo ya maridhiano kati ya Upinzani na Serikali inaongozwa na Kalonzo Musyoka wa Azimio na Kimani ichung’wa wa Kenya Kwanza.

BY MJOMBA RASHID