HabariNews

Idadi kubwa ya Wakazi Pwani yafurika Uhuru na Kazi wakilalamikia kujikokota kwa utoaji Pasipoti

Kumeshuhudiwa msongamano mkubwa katika afisi za Idara ya Uhamiaji hapa mjini Mombasa, huku idadi kubwa ya wakazi Ukanda wa Pwani ikikita kambi kutaka paspoti zao.

Wakazi hao ambao walifurika Siku ya Ijumaa katika Jumba la Uhuru na Kazi mjini Mombasa walionyesha kughadhabishwa na jinsi zoezi hilo linavyoendeshwa kwa mwendo wa kobe, wamemtaka Waziri wa masuala ya Ndani Prof. Kithure Kindiki kuingilia kati mchakato huo ili kufanikisha kupatikana kwa stakabadhi hizo.

Walidai kuwa shughuli hiyo imejawa ufisadi kwani kuna baadhi ya wananchi wanaopata paspoti zao bila kufuata taratibu, kauli iliyopingwa vikali na mkurugenzi wa idara ya uhamiaji ukanda wa pwani James Nyatigo.

”Tumekuja tangu saa kumi na moja bado hatujashughulikiwa pasipoti miaka miwili si ni kuonewa tunalilia haki zetu,kwa nini mmetuma ujumbe kuita watu kama ni za kazi gani,kama hamajajipanga hangetutumia messeji ,mmeacha watu wamesisima mpaka tumechoka.”Waliteta

Kwa upande wake James Nyatigo ambaye ni Mkurugenzi wa uhamiaji Pwani amewahakikishia wakazi hao kuwa waliopata jumbe kutoka serikali watapata paspoti zao bila wasiwasi huku akishikilia kuwa zaoezi hilo litazinduliwa rasmi Jumatatu wiki ijayo na waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki.

“Kuanzia jumatatu saa tutanza zoezi kuwapa wote waliopata ujumbe wa serikali na zoezi sawia na hili litaendelea kwenye ofisi zote za kamshina kwa mwezi mmoja tunataka kuhakikisha kuwa pasipoti zote ambazo zimetolewa zinapeanwa kwa wenyewe.”Alisema Nyatingo.

Nyatigo akiwasisitizia kuwa waliochukuliwa risiti za hii leo wote watarudi nyumbani na stakabadhi hiyo.

“Wote waliopata ujumbe tumechukua risiti zao na tutahakikisha watapata risiti zao.”Aliongeza Nyatingo.

Kufikia sasa zaidi ya watu 4800 wamepokea ujumbe za kupata paspoti zao huku ofisi ya uhamiaji pwani ikiwa na idadi ya paspoti zaidi ya 8000.

BY DAVIT OTIENO