HabariNews

Mombasa yatakiwa kujizatiti kuvutia Wawekezaji

Serikali ya kaunti ya Mombasa imehimizwa kuweka mazingira bora ili kuvutia wawekezaji wa kimataifa na wa hapa nchini.

Akizungumza na meza yetu ya habari kutoka jijini Nairobi, Mshauri mkuu wa kisiasa wa rais William Ruto, Karisa nzai alisema kuwa uzinduzi wa Eneo la Viwanda na biashara kaunti ya Mombasa unaipa kaunti hiyo fursa mwafaka ya kukuza uchumi wake.

Nzai alimpongeza rais Ruto kwa utekelezaji wa ahadi zake kwa wakazi wa Pwani kutokana na uzinduzi wa miradi ya kitaifa huku akiitaja miradi hiyo kuwa itasaidia wakaazi wa kanda ya pwani kiuchumi na pia kubuni maelfu ya ajira miongoni mwa vijana.

“Ninamshukuru rais kwa juhudi zake Kuimarisha uchumi na kutekeleza baadhi ya ajenda za wapwani, ujenzi wa wa kiwanda hiki utainua biashara nakuongeza nafasi zaidi ya ajira”

Nzai hatahivyo aliwarai wakaazi wa kanda ya pwani kuwa na subra kwani serikali ya kitaifa imeweka mikakati ya kutosha kupunguza gharama ya maisha.

BY SAMMY MWAURA