HabariNews

AMWIK Yataka Utekelezaji wa Sera Kudhibiti Dhuluma za kingono kwa Waandishi wa habari

Muunganano wa waandishi wa habari wa kike nchini AMWIK umetaka kuundwa kwa sera itakayo dhibiti maswala ya dhulma za kingono ili kuboeresha pakubwa juhudi za kukabiliana na changamoto hizo kwa waandishi wa habari.

Akizungumza na wanahabari baada ya mkutano wa kujadili sera hiyo katika kaunti ya Mombasa, afisa mkuu mtendaji wa AMWIK Patience Nyange alisema licha kuwa na sheria kadha za kukabiliana na dhulma za kingono, tasnia ya uhanahabari bado inakumbwa na dhulma hizo sio tu KWA waandishi wa kike bali wa kiume vile vile.

Kulingana na Nyange iwapo mashirika ya habari nchini yatatekeleza sera ya kudhibiti maswala ya dhulma za kingono , idadi kubwa ya matatizo hayo yatapungua kwa kiasi kikubwa akishikilia kuwa kutokuwepo kwa sera hiyo kumechangia wengi kudhohofika .

tumeamua mikakati itakuwa tofauti ,tuje tuongee nakila mtu kuweza kuelewa, ukosefu wa sera katika maeneo yetu ya kazi umefungua njia ya sisi kudhulumiwa. Hizi sera zinahitajika na zinaweza kusaidia katika kuboresha mazingira ambayo waandishi wa habari wanafayia kazi” alisema Nyange

Nyange aliwataka wanadishi wanaohisi kudhulumiwa kutosalia kimya, bali watoe ripoti ili kuweza kufanikisha vita hivyo .

Unapodhulumiwa na unyamaze basi unaendeleza dhulma, kwa hivyo tunaomba kila mmoja aweze kujitokeza yeyote Yule ambaye anafanya kazi katika mazingira ambayo hayafai aweze kuongea, aweze kujitokeza tushirikiane sisi sote tukiwa  katika vikundi mbali mbali ambavyo vimo. Tuko na mashirika mbali mbali kwahivyo wito wangu ni kwamba kwa ule yeyote ambaye amepata shida hapo mbeleni sisi tumefungua milango yetu njoo utuongeleshe tutajaribu kukusaidia kadri ya uwezo wetu” alisisitiza.

Kulingana na tafiti, visa vya dhulma za kingono katika nyanja ya uhanabari vimekua vikiongezeka kila mwaka huku wanaodhulumiwa wakishindwa kuripoti visa hivyo kutokana na hofu ya kupoteza ajira.

AMWIK hata hivyo iko katika harakati ya kuunda sera itakayongoza vyombo vya habari katika kudhibiti visa hivyo lengo kuu likiwa ni kutoa mafunzo kwa wadau wakuu wa sekta hio nchini.

BY DAVID OTIENO