HabariNews

Teknolojia Kabambe Kuzuia Ufisadi Hospitalini, huduma Zikiimarika

Kuna haja ya hospitali za umma na zile za kibinafsi kutumia vifaa vya kidigitali ili kuimarisha huduma kwa wateja wake.

Mkurugenzi Mkuu katika shirika la Smart Application Harrison Muiru aliyasema haya akidokeza kuwa hatua hiyo itapunguza donda sugu la ufisadi hasa hospitalini ambapo unatajwa kukita mzizi humu nchini.

Muiru aliitaja hatua hiyo kama njia mojawapo itakayowezesha wagonjwa kujua ni kiasi gani cha pesa wanachopaswa kutumia kwani Kila data zitahifadhiwa kwenye kifaa maalum cha kiteknolojia almaarufu kama Biometric Device.

Hali hii itasaidia kutoa huduma kwa wagonjwa huku mtambo huu ukiweka data za kila mgonjwa atakayezuru hospitalini,itakuwa anaweka kidole kwa mashini na data yake yote itakuwa inaonyesha kwa mtandano huu wa Biometric Device”.Alisema Harrison.

Kauli yake ilieungwa mkono na mwakilishi katika shirika la Smart Application ukanda wa Pwani Benjamin Sila aliyedokeza kuwa hali hio, itasaidia ukuaji wa huduma za afya hospitalini na hata kwa wagonjwa wanaotafuta matibabu mbalimbali.

Kulingana na Benjamin kifaa hicho cha teknolojia kitarahisisha huduma hospitalini ikiwa ni pamoja na kuhifadhi data ili kupunguza msongamano katika hospitali zetu au hata kwa kutumia simu na data.

“Ujumuishaji wa teknolojia utasaidia kuondoa ufisadi katika mahosipitali yetu ambapo umekuwa donda sugu,huku tukilenga hospitali nyingi zaidi ukanda huu wa pwani”.Asisitiza Benjamin.

BY EDITORIAL DESK