HabariNews

Bei ya mafuta kupanda hadi sh. 300 Kutokana na Vita vya Israel na Hamas, Waziri Chirchir asema

Vita kati ya Israel na Hamas huenda vikapelekea bei ya mafuta kupanda hadi shilingi 300 kwa lita.
Ni kauli yake Waziri wa Nishati nchini Davis Chirchir akiwa mbele ya Kamati ya Mazungumzo ya Kitaifa huko Bomas.

Kulingana na Waziri Chirchir  mzozo kati ya mataifa hayo mawili huenda ukapelekea bei ya mafuta kuongezeka kimataifa na kufikia dola 150 kwa lita. Alisema katika mapitio yajayo ya mafuta ya Mamlaka ya kudhibiti kawi na mafuta nchini, EPRA serikali italazimika kupandisha bei hio kutoka shilingi 200 iliyopo sasa.

Kwa sababu ya Vita ya Hamas na Israel inayoendelea bei ya Kimataifa ya mafuta inaweza kupanda na kufikia dola 150 kwa lita, na hiyo inamanaisha kuwa bidhaa zetu zitaongezeka kuwa shilingi 300 kwa lita. Tunatumai haitafikia huko lakini,” Alisema Waziri Chirchir.

Itakumbukwa kuwa bei ya mafuta ya awali iliyotolewa mwezi uliopita iliweka historia baada ya kugonga rekodi ya 200 kwa mara ya kwanza kwa lita.

BY MJOMBA RASHID